2013-04-26 15:12:32

Kuweni ujasiri wa kutenda makubwa lakini kw a unyenyekevu – Papa Francisko


Siku ya Alhamis, Papa pia alihimiza ujasiri wa kufanya mambo makubwa kwa unyenyekevu, na kuwa na moyo wa shukurani hata kwa mambo madogomadogo.

Papa Francisko, alihimiza hilo wakati wa homilia yake ya mapema asubuhi siku ya Alhamis, katika adhimisho la Ibada ya Misa, aliyo iongoza katika jengo la Domus Sanctae Marta, la Vatican. Na alilenga katika jinsi Wakristo wanavyo paswa kutangaza Habari Njema kama ilivyotakiwa na Yesu Mwenyewe. Homilia ilitafakari somo la Injili ya Marko, liliyosomwa wakati wa Liturujia ya Neno.
Alisema, tukishirikishana furaha ya adhimisho la Sikukuu ya Mtakatifu Marko Mwinjilisti,tunayoiadhmisha leo, Wakristu tunapaswa kuwa na ushupavu wa kutenda makuu lakini kwa uyenyekevu na moyo wa shukurani hata kwa mambo madogomadogo.

Kati ya walioshiriki katika Ibada hii ni pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya Sinodi ya Maaskofu , wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Sekretariat hiyo, Askofu Mkuu Nikola Eterovic, kulikuwepo pia kikundi kidogo cha polisi kutoka Kikosi cha ulinzi Vatican.

Homilia ya Papa Francisko ililenga zaidi Kupaa kwa Bwana Yesu, na kwamba, Kabla ya kupaa mbinguni, Yesu aliwatuma wanafunzi wake, kwenda kuhubiri Injili hadi miisho yote ya dunia, na si tu Yerusalemu au Galilaya.

Kwenda duniani kote na miisho yote ya dunia, ndio utume wa Kanisa. Kanisa linaendelea kuhubiri hili kwa kila mtu, duniani kote. Na haendi peke yake lakini na Yesu. Na hivyo ndivyo, Wakristu wa mwanzo, walivyokwenda kuhubiri kila mahali , na Bwana kutenda pamoja nao. Bwana hufanya kazi na wale wote wanaoihubiri Injilii yake kwa moyo wa kweli na kuliishi neno lake. Na hiyo ndiyo sura ya utendaji wa Mkristu, unavyotakiwa uwe na ni wito Kikristo! Daima zaidi na zaidi, zaidi na zaidi, zaidi na zaidi, daima na kuendelea kuihubiri Injili.
Papa aligeukia pia somo kutoka Barua ya Kwanza ya Mtakatifu Petro, akisema, Mtakatifu Petro, anafafanua mtindo wa mahubiri ya kikristo kwamba, unapaswa kuwa wa unyenyekevu, kama huduma, upendo wa kidugu, ambamo Bwana anaushinda ulimwengu! Ni kuhubiri ushindi duniani. Mkristu , iliendelea Papa, anaitangaza Injili kwa ushuhuda wa maisha yake , badala ya maneno. Na pamoja na sura mbili kama Mtakatifu Thomas Aquinas, alivyosema, akiwa na moyo mkuu usioogopa kutenda makuu, wenye kuwa na ushupavu wa kusonga mbele, lakini wakati huohuo akiwa mnyenyekevu katika kuzingatia hata madogomadogo. Maisha kama hayo n i maisha matakatifu.

"Wakati sisi tunatembea katika njia ya ujasiri na unyenyekevu, ambamo hatuogopeshwi na mambo makubwa katika upeo wa macho , pia tunazingatia mambo madogomadogo, kwa unyenyekevu na matendo ya huruma katika maisha ya kila siku. Na Bwana unatuimarisha kwa neno lake na hivyo tunawezeshwa kusonga mbele. Furaha ya ushindi wa Kanisa ni ufufuo wa Yesu, ulioanza na mateso ya Msalaba.

Leo hii tunamwomba Bwana atufanye kuwa wamisionari wa Kanisa, Mitume wa Kanisa , katika roho hii ujasiri mkubwa, na pia unyenyekevu mkubwa. Bwana na atujalie hilo. Papa alimazlia.








All the contents on this site are copyrighted ©.