Kikosi kazi cha Jeshi la Kimataifa kinashutumiwa kwa kuhusika na mauaji ya kinyama
Kaskazini mwa Nigeria
Mauaji ya kutisha yaliyotokea hivi karibuni Kaskazini mwa Nigeria kwa kupelekea watu
185 kupoteza maisha yao, kitendo ambacho kilishutumiwa na Jumuiya ya Kimataifa yalisababishwa
na operesheni maalum iliyofanywa na Kikosi Kazi cha Jeshi la Kimataifa linaloundwa
na wanajeshi kutoka: Nigeria, Chad, Niger na Cameroon waliopewa dhamana ya kulinda
usalama kuzunguka Ziwa Chad.
Kikosi hiki kimeshutumiwa vikali kwa kutumia
nguvu kupita kiasi kujibu mashambulizi yaliyoelekezwa kwao kutoka kwa Kikundi cha
Boko Haram. Mashahidi wanasema kwamba, wanajeshi waliamua kufanya oporesheni hii baada
ya kuona kwamba, kuna baadhi ya wananchi waliokuwa wanatoa hifadhi kwa wanajeshi wa
Kikundi cha Boko Haram. Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ameamua kufanya uchunguzi
wa kina ili kubaini ukweli wa mambo.