Tafakari juu ya Mzawa wa Bikira Maria- Padre Darius Kowalczyk
Padre Darius Kowalczyk , katika tafakari yake ya 26 juu ya Katekismu Mpya ya Kanisa
Katoliki, wiki hii ameangalisha katika Nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu , ambayo tunakiri
Bwana kumwilishwa, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. . Baba Mwana wa milele alitungwa
mimba ndani ya tumbo la Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa. Na
hivyo , Kateksimo inatufahamisha juu ya msingi wa imani kwa Mwana aliyezaliwa na Bikira
Maria, Yesu Kristo (n. 487). Kwa hiyo, Kanisa, linakiri kwamba Yesu Kristo ni binadamu
Mtakatifu mwenye asili mbili: asili ya Mungu na asili ya ubinadamu. Hivyo basi Kanisa
linakiri kwamba "Maria ni kweli Mama wa Mungu (Theotokos)(CCC, 495). Na hivyo tunamzungumzia
Mama wa Mungu kwa sababu Mungu akawa mtu kwa wakati fulani katika historia ya binadamu
kupitia kwake Bikira Maria. Kanisa pia humwadhimisha Maria kama "Bikira milele,"likikiri
kwamba ubikira wa Maria ni wa kweli na ni wa daima. Kateksimu inaeleza kwamba, kutunga
mimba katika hali ya ubikira ni alama hai kwamba, ni kweli alikuwa Mwana wa Mungu"
(n. 496). Basi, ubikira wa Maria hudhihirisha mpango Mungu wa kumwilisha mwana wake
(n. 503). Vivyo hivyo, ubikira, unakuwa ni ishara inayo onyesha kuzaliwa kwetu upya
katika maisha ya milele, si kwa mapenzi ya mwili wala kwa mapenzi ya mtu, bali mapenzi
ya Mungu" (Yn 01:13) (cf. CCC, 505).
Malaika alimsalimu Mariaā€¯ umejaa neema".
Katika mapito yote ya uwepo wa Kanisa, limeongozwa na Roho Mtakatifu ili ukweli
wote ujulikane kwamba Bikira Maria alijawa neema kamili , ikionyesha pia Maria hakuwa
na dhambi. Mama wa Mungu - katika mtazamo wa mastahili ya Mwana wake , alikingiwa
kila asili ya doa la dhambi ya asili" (CCC, 491). Kwa njia hii Mungu alimchagua
Maria kuwa Mama wa Mwana wake, na si Maria aliyefanya uchaguzi huo. Na moja ya majibu
yake yanayonyesha kweli huo, Mimi ni mjakazi wa Bwana, basi, na iwe kwangu kama ulivyosema
(Lk 1.37-38).