Padre Pierrabattista Pizzaballa, Mkuu wa Jumuiya ya Wafransikani, yenye dhamana ya
Ulinzi katika maeneo Matakatifu katika Nchi Takatifu, hivi karibuni ilitoa wito nguvu
kwa ajili ya ufumbuzi wa mgogoro wa Syria. , Akihojiwa na Redio Vatican,juu ya
mgogoro huo na utekwaji wa nyara wa Maaskofu wawili, ameonyesha imani yake kwamba,
utekwaji nyara wa Maaskofu hao wawili, wa Kanisa la Kiotodosi , kimsingi umemotisha
na sababu za kiuchumi. Maaskofu waliotekwa nyara ni wa eneo la Aleppo, Askofu Mar
Gregorios Ibrahim wa Kanisa la Kiotodosi Syria na Askofu Paul Yazigi wa Kanisa la
Kiotodosi la Kigriki la Antokia. Na dreva wao aliuawa wakati wao wakiendelea kutoa
huduma za kibinadamu wa wahitaji Syria. Padre Pizzaballa, anasema, kwa bahati
mbaya, pamoja na vita vinavyoendelea, pia kuna aina nyingi za magenge na makundi
ya wahalifu ambao wanautumia mwanya wa machafuko kujinufaisha kwa namna moja au nyingine
, kama pia inavyoonekana Iraq. Na pia sababu za kidini au ushabiki wa kupindukia
, haziwezi kuondolewa, lakini hasa zaidi ya yote ni sababu za kiuchumi. Na akizungumzia
matumaini ya jumuiya yake katika kupata jawabu la kusitisha ghasia katika taifa la
Syria, aliitaja jumuiya ya kimataifa kwamba, itaweza kusitisha upelekwaji wa silaha
na utoaji wa ruzuku kwa waasi na serikali,kigezo kikubwa kinachoendeleza ghasia hizo
siku hadi siku. Aliendelea kugusia madhara makubwa ya kiuchumi yaliyosababishwa
na matokeo ya vita vya wenyewe, yaliyovuka hata mipaka ya Syria na kuingia katika
nchi jirani, ambako mamilioni ya Wasyria wanaishi kama wakimbizi. Watu hao wamepoteza
matumaini ya kuajiriwa, mbele yao kumefunikwa na giza nene dhidi ya ajira, licha
ya kukosa makazi na mahitaji ya msingi. Na hivyo , pamoja na wakimbizi, pia kuna
waasi, na wahafidhina, wanaoeneza kama moto nyikani, uzushi wa kila aina, ambayo
kwa bahati mbaya umeshuhudiwa pia katika taifa la Iraq na mahali pengine Mashariki
ya Kati.
Padre Pizza balla alimalizia maelezo yake na matumaini ya kibiblia.
Na kwamba, ni muhimu kwa Wakristo kutoihama Syria , bali wabaki na imani hai katika
kuitetea imani yao kwa nchi alimozaliwa Yesu Kristu