Wanasiasa wa Italia wanapaswa kuwajibika kwa ajili ya mafao ya wengi!
Rais Giorgio Napolitano baada ya kula kiapo na kulihutubia Bunge la Italia, hapo tarehe
22 Aprili 2013 anakuwa ni Rais wa kumi na mbili ambaye amebahatika kuiongoza Italia
kwa vipindi viwili, jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Italia.
Rais
Napolitano mwenye umri wa miaka 88 katika hotuba yame anawataka wanasiasa wa Italia
kutekeleza wajibu wao kikamilifu wakizingatia nidhamu, umoja wa kitaifa na mafao ya
wengi ili kuwajengea tena matumaini mapya wananchi wa Italia ambao wanaendelea kukata
tamaa kutokana na athari za myumbo wa uchumi kimataifa pamoja na kinzani za kisiasa.