2013-04-23 15:19:52

Haiwezekani kudai kuishi na Kristu na huku uko nje ya Kanisa- Papa


Jumanne hii 23 Aprili, maelfu ya salaam za matashi mema zimemiminika kwa Papa Francis, kwa ajili ya adhimisho la Siku Kuu ya wajina wake Mtakatifu George. Papa Francis, jina lake jingine ni George Mario Bergoli.
Kwa ajili ya Siku Kuu hii, Mapema Jumanne, Papa aliadimisha Ibada ya Misa Katika kikanisa cha Mtakatifu Paulo cha mjini Vatican , akiwa na Makardinali wanaoishi Roma. Katika Ibada hiyo, Papa aliwashukuru Makardinali kwa kushirikiana nae katika adhimisho hili na kwa mapokezi na ukaribu wao, wanaounyesha tangu alipochaguliwa kuwa Papa 19 March mwaka huu. Alisema, anajisikie vyema kuwa karibu nao.
Akizungumza juu ya masomo ya siku, aliireja ari ya wakristu wa mwanzo katika kuieneza Injili, licha ya kukabiliana na katika kipindi cha mateso yaliyotaka kuvunja asili ya utume wa kimisionari wa Kanisa" wa kuieneza Injili katika maeneo ya Foinike, Kupro na Antiokia. Wakristu hao wa mwanzo, walijawa na ari ya kitume, na imani ni hivyo kutawanyika huko na kule wakiitangaza Injili. Somo la Injili lililoonyesha, ndivyo ilivyokuwa pia kwa Wayunani, na wapagani. Ilikuwa ni hatua makini kufanikisha mpango wa Roho Mtakatifu. RealAudioMP3







All the contents on this site are copyrighted ©.