2013-04-22 11:01:42

Salaam za Matashi Mema ya Papa Francesco kwa Rais Mpya wa Italia


Jumamosi mara baada ya Rais Giorgio Napolitano, kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Papa Francesco, alipeleka salaam zake za matashi mema kwa Rais huyo kwa njia ya telegram.
Papa Francesco, katika salaam hizo ameonyesha heshima na shukurani zake za dhati kwa Rais Giogio Napolitano, kuchaguliwa tena kuliongoza Taifa la Italia kisiasa. Na pia ameonyesha matumaini yake kwamba, ataendelea kutembea katika mwanga wa busara na ushirikiano mzuri na wakuu wote, katika huduma yao kwa kila binadamu na taifa pendwa la Italia.
Na mwisho alitoa baraka zake za kitume, akimtakia moyo wa kujenga mustakabali wa maelewano, mshikamano na tumaini jema.








All the contents on this site are copyrighted ©.