Yesu anachokitaka kutoka Kwenu : Ni kuwa wachungaji wenye huruma na si watendaj, Papa
amewaasa Mapadre wapya. Jumapili iliyopita, ambayo ilikuwa ni Adhimisho la 50
la Siku ya Dunia ya Kuombea Miito duniani , adhimisho lililoongozwa na Mada Kuu” Miito
alama ya Tumiani lililosimikwa katika Imani “, Papa Francisko, aliongoza Ibada ya
Misa ambamo alitoa daraja la Upadre kwa waseminaristi kumi wa Jimbo la Roma. Ibada
hiyo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, majira ya asubuhi. Mapadre
hao ni wahitimu kutoka Seminari Kuu ya Jimbo la Roma , Seminari inayosimamiwa na Jumuiya
ya Njia ya Ukatukumeni Mpya , Mama wa Mkombozi na Seminari ya Upendo Mtakatifu. Papa
Francesco, katika homilia ya wakati wa kuwaweka wakfu Mapadre wapya, alielenga zaidi
katika moja ya misingi ya ukuu wa Papa kama Askofu wa Jimbo la Roma, katika Upadirisho
huo. Na aliendelea kutafakari juu ya sakramenti ya Upadre akisema muda si mrefu
watakuwa wakiwahudumia watu wa Mungu kama Makuhani Wakuu wa Kristu , na hivyo aliwataka
daima kuwa wachungaji wenye huruma kwa watu na si tu kuwa wasimamizi au mameneja.
.
Mandhari ya miito, ilitawala katika hotuba za Papa alizozitoa hata baadaye
wakati wa Sala ya Malkia wa Mbungu, iliyohudhuriwa na watu wanao kadiriwa kufikia
70 elfu, waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, majira ya
saa sita za mchana. .
Papa Francesco, alibainisha kuwa "wakati mwingine Yesu
anatuita na anatualika kumfuata, lakini inaweza kutokea, tukashindwa kumtambua kuwa
Yeye Yesu. Na hivyo alihimiza waumini na hasa vijana kuisikiliza kwa makini sauti
ya Kristo katikati katika mawazo, na hasa katika harakati za maisha yanayotaufa ukweli
adilifu. Aliwasihi vijana kwa ujasiri, kumsikiliza Bwana.
Pia alibainisha
kuwa "nyuma na mbele ya kila wito wa ukuhani au maisha ya wakfu, daima husindikizwa
na nguvu ya maombi, iwe kutoka kwa mtu binafsi, bibi, babu, mama, baba, shangazi
au jamii ya waumini kwa ujumla ". Sala inayoomba waamini kila mahali kuongeza juhudi
zaidi katika kuombea Miito , ambayo hata leo hii, ni hitaji muhimu, ili wafanyakazi
katika shamba la Bwana, waweze kuongezeka.