Tarehe 22 Aprili 2013, dunia inafanya adhimisho la 43 la Siku ya Mazingira Duniani
, adhimisho linalo wahusisha zaidi ya watu bilioni moja duniani kote. Ni maadhimisho
ya kila mwaka, yenye kuonyesha utendaji mbalimbali, kwa ajili ya kuonyesha utetezi
na ulinzi mazingira.
Papa Francis , hapo tarehe 19 March mwaka huu, akitoa
hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kama Papa , alionyesha kujali umuhimu
wa kutetea na kutunza mazingira katika asili yake. Hoja iliyogusa watetezi na walinzi
wote wa viumbe na mazingira asilia. Aliwatahadharisha wote wale wenye nafasi za
uongozi, iwe kisiasa, kiuchumi, au kijamii, wake kwa waume wenye mapenzi mema, kuwa
watetezi na walinzi wa viumbe, walinzi wa mpango wa Mungu, ulio andikwa katika asili
yote, walinzi wa mmoja kwa mwingine na mazingira ".
Adhimisho la mwaka huu
la Siku ya Dunia 2013 linaoongozwa na Kaulimbiu : "uso wa Mabadiliko ya Tabianchi",
na imechaguliwa kwa lengo la kutoa angalisho makini zaidi , katika athari zinazo
zidi kuleta mabadiliko katika tabia nchi , kama inavyoshuhudiwa na mtu binafsi na
dunia kwa ujumla.
Adhimisho hili huratibiwa na Asasi ya Mtandao wa Siku ya
Dunia, kwa kushirikiana na wabia wengine katika kazi za kutetea na kudumisha mazingira
bora duniani, Asisi inayoongozwa na Rais Bibi Kathleen Rogers. Bibi Rogers mapema
Jumanne, akizungumza katiak mahojiano na Linda Bordoni wa Redio Vatican, alionyesha
tumaini lake kubwa, alilolijenga kwa Papa Francesco,katika kupambana na athari za
mabadiliko ya tabia nchi na ulinzi wa dunia na viumbe wake. Amesema,”Hotuba ya kwanza
ya Papa Francesco, ili ashiria mengi, juu ya mazingira asilia ya dunia na wanyama.
Na pia, uzoefu wake, yeye mwenyewe katika kuyaishi maisha ya kawaida , kama kutumia
usafiri wa umma, kujipikia mwenyewe, na maisha yake ya kawaida, yanaoonyesha kwamba,
kila mtu anaweza kuziishi nyayo hizo za maisha ya kawaida lakini endelevu. Bi Rogers,
aliendelea kuionyesha imani yake kwa Papa Francesco kwamba, kwa ukuu wa nafasi yake,
anao uwezekano wa kuiongoza dunia katika utendaji wa kidharura kwa ajili ya kuikoa
dunia dhidi ya shinikizo la kidharura za mabadiliko ya tabia nchi, kwa sababu kila
mtu humsikiliza.
Anaamini Papa Francesco , anao uwezo kuchukua jukumu hili
kubwa kwa kuwa yeye mwenyewe anajali maskini, na tayari ana wasiwasi kuhusu athari
za mabadiliko ya tabia nchi yanavyo lemea watu maskini, na hasa katika muono kwamba,
tayari aliyaishi maisha hayo na hivyo anaizungumzia hali aliyoiishi katika maisha
yake ya kila siku, kama pia ambavyo tayari, anafahamika kuwa mtetezi mashuhuri katika
masuala ya usawa wa kijinsia, na viongozi wa serikali na mashirika humsikiliza.