2013-04-22 09:48:54

Maafa China: zaidi ya watu 188 wamepoteza maisha na wengine 11,000 wamejeruhiwa


Serikali ya China siku ya Jumatatu, tarehe 22 Aprili 2013 imefanikiwa kufikisha msaada wa dharura kwa watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi mwishoni mwa juma na hivyo kusababisha zaidi ya watu 188 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 11,000 kujeruhiwa vibaya katika Jimbo la Sichuan.

Msaada wa dharura umechelewa kufika kwenye eneo la tukio kutokana na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja na maporomoko ya udongo. Juhudi zinaendelea kufanywa na waokoaji sanjari na ugavi wa chakula, maji na mahitaji mengine ya msingi eneo la vijijini huko Sichuan, China.







All the contents on this site are copyrighted ©.