2013-04-19 08:18:59

Papa kutoa Daraja Takatifu la Upadre kwa Mashemasi 10 mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo wa sita alipozindua rasmi Siku ya Kuombea Miito Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka katika Jumapili ya Nne ya Kipindi cha Pasaka, anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika Ibada hii anatarajiwa pia kutoa Sakramenti ya Daraja Takatifu la Upadre kwa Mashemasi kumi.

Taarifa kutoka kwa Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa Monsinyo Guido Marini zinaonesha kwamba, kuna Mashemasi wanne kutoka Seminari kuu ya Kipapa ya Roma. Mashemasi wawili ni wale wanaotoka kwenye Shirika la "Divino Amore" wakati ambapo Mashemasi wengine wanne wanatoka Seminari kuu ya Jimbo inayojulikana kama "Redemptoris Mater". Kimsingi, Mashemasi watakaopewa Daraja Takatifu la Upadre kwa mara ya kwanza kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko wanatoka: Argentina, Croatia, India na Italia.

Ibada ya Misa takatifu inatarajiwa kuanza rasmi saa 3:30 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.