2013-04-17 15:08:42

Maelfu wamzika Margaret Thatcher- Uingereza.


Maelfu ya mashabiki wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1979 hadi 1990, Magaret Thatcher, mapema Jumatano hii, walimiminika katika Kanisa kuu la Westminster , mjini London, kuhudhuria ibada ya wafu na maziko ya Waziri Mkuu huyo. Margret Thatcher , alifariki Jumatatu ya tarehe 8 April, kwa maradhi ya kiharusi. Malkia wa Elizabeth 11, alikuwa kati ya wanasiasa mashuhuri wa Uingereza na kutoka pande mbalimbali za dunia waliohudhuria Ibada na mazishi hayo.
Asubuhi na mapema, maelfu ya watu walijipanga katika mitaa ya jiji la London ambako jeneza la Marehemu Margaret Thatcher, likiwa limebebwa katika gari maalum la farasi , lilipitishwa kwa heshima zote za taifa la Uingereza ,kuelekea katika Jengo mashuhuri la Kisiasa nchini Uingereza, kukamilisha safari yake ya kabla ya mazishi. Mabango mengi yaliyokuwa yamebebwa , yalikuwa na maneno ya sifa kwa Margaret Thatcher , ingawa pia kulikuwa na wachache waliomkashifu.
Na wengi waliohojiwa kuhusu maziko haya wameonyesha kutofurahishwa na matumizi ya dola millioni 15 za Marekani za walipa kodi , kutumika katika mazishi haya ya kifahali.
Margaret Thatcher amepewa heshima ya kuangwa kwa mlio wa bunduki uliosikika kila dakika tokea mnara wa London, na mlio wa kengere kubwa ya jiji hilo.
Katika kipindi cha miaka 150, Marehemu Margaret Thatcher, anakumbukwa katika historia ya Uingereza, kuwa mwanamke wa kwanza kutumikia kwa muda mrefu kama Waziri Mkuu wa Uingereza. Na aliweza kufanikisha mengi , ikiwemo ushindi wa ejshi la Uingereza latola vota ya Falklands ya mwaka 1982.








All the contents on this site are copyrighted ©.