2013-04-17 15:25:25

Maadhimisho ya Siku ya Dunia dhidi ya watoto kutumikishwa kama watumwa


Jumanne , tarehe 16 April , kama ilivyo kwa tarehe hiyo,kila mwaka, ilikuwa ni Siku ya Dunia dhidi ya watoto kutumikishwa kama watumwa. Dunia kote kuna watoto zaidi ya millioni mia nne, ambao ni sawa na asilimia kumi ya watoto wote duniani, hulazimishwa na watu wazima, kufanyakazi ngumu na ujakazi.
Tarehe hii ilitengwa na jumuiya ya kimataufa tangu mwaka 1995 , baada ya mtoto wa kiume wa miaka 12 wa Pakistani, Iqbal Masih, kufariki kwa sulubu za kazi alizoanza kutumikishwa tangu akiwa na umri wa miaka 4, baada ya kuuzwa na baba yake, ili aweza kulipa madeni ya familia yake.
Matukio haya ya kusikitisha ya watoto kutumikishwa kazi ngumu , ujakazi na sulubu au kulazimishwa kuwa ombaomba, au kuingizwa katika mfumo wa biashara haramu ya ukahaba, zimeshamiri hasa katika mataifa mengi ya Kusini mwa tufe la dunia , hali inayoibukia pia katika mataifa kadhaa ya Ulaya katika nyakati hizi.
Kwa mujibu wa Takwimu zililotolewa na Shirika la Okoa Watoto la Uingereza, kati ya mwaka 2008 hadi 2010 , watoto 23, 932 , waliuzwa katika biashara haramu ya binadamu , kukiwa na ongezeko la asilimia 13 , ambamo watoto wengi, huishia kukamatwa katika vitendo vya uhalifu, ombamba na ufuska.
Taarifa hiyo , inataja mataifa nyenye utajiri mwingi wa madini kama Brazil na Benin, watoto wengi hutumikishwa katika migondi, wakati katika mataifa nyenye kuwa na mizozo ya kivita ya muda mrefu kama ilivyo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watoto wengi, wamesajirishwa katika vikosi vya waasi , kama Maaskari wapiganaji. Na mataifa fukara zaidi kama Haiti, familia fukara huuza watoto wao kama tumaini pekee ya kuikoa familia na hali ngumu ya maisha au kwa nia za kulipa madeni.
Hali hii inatajwa kuwa ni aibu kubwa katika dunia ya leo inayotajwa kuwa dunia iliyostaraabika.








All the contents on this site are copyrighted ©.