2013-04-16 10:27:08

Imegota miaka 86 tangu alipozaliwa Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI


Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, tarehe 16 Aprili 2013 anaadhimisha kumbu kumbu ya miaka 86 tangu alipozaliwa. Papa mstaafu Benedikto wa kumi na sita kwa sasa bado anaendelea kuishi Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo, iliyoko nje kidogo ya Mji wa Roma.

Tangu alipong'atuka kutoka madarakani amekuwa akitumia muda wake mrefu kwa ajili ya kusali, kutafakari, kujisomea vitabu pamoja na kusikiliza muziki. Watu wengi wanamkumbuka kutokana na ujasiri wake aliouonesha kwa kung'atuka kutoka madarakani kwa uhuru na utashi kamili, ili kutoa nafasi kwa ajili ya kiongozi mwingine atakeendeleza dhamana ya kuliongoza Kanisa kwa ari na moyo mkuu.







All the contents on this site are copyrighted ©.