2013-04-13 15:15:14

Papa aunda tume ya Makardinali kuangalia uongozi wa Kanisa la Kiulimwengu


Baba Mtakatifu Francisko kwa kuzingatia ushauri uliotolewa na Makardinali katika mikutano yao elekezi iliyofanyika kabla ya uchaguzi wa Papa Mpya ameamua kuunda Tume ya Makardinali watakaomshauri kuhusu shughuli za uongozi wa Kanisa la Kiulimwengu pamoja na kupembua kwa kina na mapana Waraka wa Kichungaji Pastor Bonus, Mchungaji mwema unaohusiana na masuala ya Ofisi za Vatican.

Kwa mara ya kwanza tume hii itakutana kuanzia tarehe 1- 3 Oktoba 2013. Tangu wakati huu, Baba Mtakatifu Francisko ataanza kuwasiliana moja kwa moja na wahusika kwa ajili ya kupata ushauri makini.







All the contents on this site are copyrighted ©.