Endeleeni kumwombea Papa Francisko katika maisha na utume wake!
Kardinali Polycarp Pengo, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika
na Madagascar, SECAM anaendelea kumwombea Baba Mtakatifu Francisko ili Mwenyezi Mungu
aweze kumlinda na kumwimarisha katika imani, matumaini na mapendo anapotekeleza utume
wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.
Anamwombea
afanikishe malengo na nia njema zilizoko moyoni mwake, lakini zaidi aweze kuwaimarisha
ndugu zake katika imani kwa Kristo na Kanisa lake, hasa zaidi maskini, wanaosukumizwa
pembezoni mwa Jamii na wote waliokata tamaa kutokana na madhulumu mbali mbali.
Kardinali
Polycarp Pengo anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kumwombea
Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake.