2013-04-12 10:11:19

Sudan ya Kusini yatembelewa kwa mara ya kwanza na Rais Omar Al Bashir


Rais Omar Al Bashir wa Sudan Kongwe, Ijumaa, tarehe 12 Aprili 2013, kwa mara ya kwanza tangu Sudan ya Kusini ilipoamua kujitenga na kuwa nchi Huru kunako mwaka 2011 amewasili mjini Juba, Sudan ya Kusini.

Lengo la ziara hii ya kikazi wanasema wachunguzi wa masuala ya kisiasa ni kutaka kurudisha hali ya kawaida kati ya nchi hizi mbili ambazo kwa siku za hivi karibuni zilijikuta zikiingia katika kinzani kuhusu uzalishaji wa nishati ya mafuta.

Suluhu ya mgogoro huu ilifikiwa hapo tarehe 12 Machi 2013 kwa makubaliano kwamba, uzalishaji na usafirishaji wa nishati ya mafuta kutoka Sudan ya Kusini uendelee kama kawaida.







All the contents on this site are copyrighted ©.