2013-04-10 11:56:16

SIGNIS kufanya mkutano wake mkuu mjini Beirut, Lebanon kama alama ya mshikamano wa upendo


Shirikisho la Vyama vya Mawasiliano vya Kanisa Katoliki Duniani, SIGNIS, litakuwa na mkutano wake mkuu utakaofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 23 Oktoba 2013 mjini Beirut, Lebanon; wakiongozwa na kauli mbiu "Vyombo vya Habari kwa ajili ya utamaduni wa amani, kutengeneza taswira kwa kushirikiana na Kizazi Kipya". Mkutano huu unafadhiliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii pamoja na Radio Vatican.

Jumatatu, tarehe 15 Aprili 2013, Askofu mkuu Claudio Maria Celli pamoja na Padre Federico Lombardi watakuwa ni kati ya wawezeshaji wakuu wakati SIGNIS itakapokuwa inazungumza na Waandishi wa Habari hapa mjini Vatican. Vatican inaipongeza SIGINIS kwa uamuzi huu wa busara kama kielelezo cha mshikamano na wananchi wanaoendelea kuteseka huko Mashariki ya Kati.

Itakumbukwa kwamba, hata Tafakari ya Njia ya Msalaba kwa mwaka 2013 kuzunguka Magofu ya Colosseo Ijumaa kuu jioni, iliandaliwa na vijana kutoka Lebanon.







All the contents on this site are copyrighted ©.