2013-04-10 15:49:19

Papa Francisko aguswa na mateso ya wananchi wa Iran waliokumbwa na tetemeko la ardhi


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 10 Aprili 2013, ameonesha masikitiko na mshikamano kwa wananchi wa Iran ambao, Jumanne tarehe 9 Aprili 2013 walikumbwa na tetemeko la ardhi lililosababisha maafa makubwa katika maisha na uharibifu wa miundo mbinu. Baba Mtakatifu anawaombea wote waliofariki dunia na majeruhi anawatakia uponaji na afya njema na kwamba, anawakumbuka wote waliofikwa na maafa haya.

Taarifa kutoka katika vyombo vya habari inaonesha kwamba, hadi kufikia Jumatano tarehe 10 Aprili 2013 asubuhi zaidi ya watu 40 walikuwa wamekwisha poteza maisha na wengine 850 wamejeruhiwa vibaya katika mji wa Dashti, nchini Iran. Miundo mbinu mingi imeharibiwa kwenye Kijiji cha Chahgah, kilichoko karibu na mji wa Dashti.







All the contents on this site are copyrighted ©.