2013-04-09 15:27:18

Uhuru Kenyatta aapishwa kuwa Rais wa nne wa Kenya



Viongozi kadhaa kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika, Jumanne tarehe 9 Aprili 2013 amekusanyika mjini Nairobi kushuhudia Rais Uhuru Kenyatta (51) akiapishwa kuwa ni Rais wa nne wa Kenya, baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu Bwana Raila Odinga, kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Kenya, hapo tarehe 4 Machi 2013.

Ni matumaini ya wapenda haki na amani Barani Afrika kwamba, sasa wananchi wa Kenya wataendelea kudumisha misingi ya haki, amani na utulivu kwa ajili ya ustawi na maendeleo yao. Kati ya vipaumbele vya kwanza vinavyopaswa kufanyiwa kazi wanasema baadhi ya wananchi wa Kenya ni upatanisho, umoja na mshikamano wa kitaifa.







All the contents on this site are copyrighted ©.