2013-04-09 09:10:53

Papa atuma salam za rambi rambi kufuatia kifo cha Margaret Thatcher


Baba Mtakatifu Francisko amemtumia salam za rambi rambi Waziri mkuu wa Uingereza Bwana David Cameron, kufuatia kifo cha Baroness Margaret Thatcher aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

Katika ujumbe uliondikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican, Baba Mtakatifu anatambua fadhila za kikristo zilizojionesha kwa namna ya pekee katika utumishi wake kwa umma pamoja na kusimama kidete kuendeleza uhuru miongoni mwa Familia ya Kimataifa.

Baba Mtakatifu anaiombea roho ya Marehemu Magret Thatcher huruma ya Mungu, anapenda pia kuihakikishia Familia na wananchi wa Uingereza kwa ujumla wao kwamba, yuko pamoja nao kwa njia ya sala. Anawapatia baraka zake za kitume wote walioguswa na msiba huu.







All the contents on this site are copyrighted ©.