2013-04-06 08:02:21

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Asiyezaliwa, tarehe 8 Aprili 2013


Shirika la kutetea uhai Tanzania, "Pro Life Tanzania" tangu mwaka 2002 limekuwa likiadhimisha Siku ya kutetea uhai. Kunako mwaka 2007 Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania likatangaza kwamba, Domenika kabla ya Siku kuu ya Bikira Maria kupaswa habari kuwa atakuwa Mama wa Mungu, iadhimishwe kitaifa siku ya mtoto asiyezaliwa. RealAudioMP3

Hii ni siku ya kukumbuka maajabu ya Mungu ili kusimama kidete kulinda, kutetea na kuenzi Injili ya Uhai dhidi ya utamaduni wa kifo. Kwa mwaka huu, Siku kuu ya Bikira Maria kupashwa habari inafanyika, Jumatatu tarehe 8 Aprili 2013

Ifuatayo ni tafakari ya kina iliyotolewa hivi karibuni na Ndugu Emil Hagam, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutetea uhai Tanzania, kama inavyosomwa kwako ndani ya Studio za Radio Vatican na Padre George wa Bodyo.







All the contents on this site are copyrighted ©.