Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kukutana na Papa Francisko tarehe 9 Aprili 2013
Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa, Jumanne tarehe 9 Aprili 2013 kukutana na kuzungumza
na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon hapa mjini Vatican. Habari hizi
zimethitishwa pia na Idara ya habari ya Vatican. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa
viongozi hawa wawili kukutana na kuzungumza kwa pamoja tangu Baba Mtakatifu Francisko
alipochaguliwa hivi karibuni kuliongoza Kanisa Katoliki.