2013-04-06 08:15:12

Cor Unum yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko nchini Argentina


Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki, Cor Unum, kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, limetuma kiasi cha dolla za kimarekani 50,000 ili kusaidia juhudi za kuokoa maisha ya watu waliokumbwa na mafuriko makubwa hivi karibuni Jimboni La Plata, Argentina.

Hiki ni kielelezo cha mshikamano wa upendo na watu walioathirika kutokana na mafuriko hayo ambayo yamesababisha maafa makubwa na uharibifu wa miundo mbinu. Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki Argentina liko mstari wa mbele kusaidia kutoa msaada wa dharura kwa watu walioathirika zaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.