2013-04-04 10:27:41

Papa Francisko atuma ujumbe wa mshikamano na wananchi wa Argentina waliokumbwa na mafuriko


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa wananchi wa Argentina waliokumbwa na mafuriko makubwa mjini Buenos Aires, yaliyopelekea zaidi ya watu 60 kupoteza maisha na maelfu ya watu kukosa mahali pa kuishi pamoja na miundo mbinu mbali mbali kuharibiwa vibaya.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu mkuu Mario Aurelio Poli wa Jimbo kuu la Buenos Aires. Baba Mtakatifu anasema, anapenda kuwaonesha mshikamano wake wa dhati wakati huu wanapokabiliana na hali ngumu ya maisha. Anawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kuonesha mshikamano wa upendo na wote walioathirika kwa kuwapatia msaada wa hali na mali.









All the contents on this site are copyrighted ©.