Mungu anakupenda, hakuna sababu ya kuogopa kumpenda!
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya jamii maarufu
kama twitter anawambia kwamba, Mungu anawapenda binadamu. Hakuna sababu ya kuogopa
kumpenda Mungu. Waamini wanaalikwa kwa namna ya pekee kukiri imani yao kwa vinywa,
lakini zaidi kwa njia ya mioyo, maneno na matendo yanayodhihirisha upendo.