2013-04-03 12:09:54

Uvuvio na ukweli ni mada inayopembuliwa wakati wa Mkutano mkuu wa Mwaka wa Tume ya Kipapa ya Biblia


Tume ya Kipapa ya Biblia itakuwa na mkutano wake mkuu wa mwaka kuanzia tarehe 8 hadi 12 Aprili 2013 utakaofanyika kwenye Domus Sanctae Marthae chini ya uongozi wa Kardinali Gerhard Ludwig Muller, Rais wa Tume na Padre Klemens Stock, Katibu mkuu ambaye atasimamia kazi za mkutano mkuu.

Katika mkutano huu, wajumbe wanatarajiwa kukamilisha tafakari kuhusu "Uvuvio na Ukweli wa Biblia". Kwa miaka kadhaa, wajumbe wa Tume hii ya Kipapa wameelekeza nguvu zao zaidi ili kufanya upembuzi yakinifu ili kutambua ni kwa kiasi gani uvuvio na ukweli unajionesha katika vitabu mbali mbali vya Maandiko Matakatifu.

Lengo la tafakari hii ya kina ni kutaka kutoa mchango chanya ili kuwa na uelewa mpana zaidi juu ya maudhui ya uvuvio na ukweli, ili Neno la Mungu liweze kupokelewa na waamini wote kwa kutambua zawadi hii kubwa ambayo kwa njia yake, Mwenyezi Mungu anawasiliana na watu na kuwaalika kujenga umoja pamoja naye!







All the contents on this site are copyrighted ©.