2013-04-02 09:30:03

18 wamenusurika kwenye ajali ya Jengo Dar es Salaam


Taarifa ya Shirika la Habari la Reuters inaonesha kwamba, hadi kufikia tarehe Mosi Aprili 2013, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na kuangukiwa na ghorofa Jijini Dar es Salaam kwa sasa imefikia watu 36.

Juhudi za kuendelea kufukua kifusi kwa matumaini ya kupata miili mingine iliyofukiwa sehemu hii yanazidi kufifia kila siku. Taarifa ya Jeshi la Polisi inaonesha kwamba, kuna watu 18 walionusurika kwenye ajali ya kuporomoka kwa Jengo lenye ghorofa 16 kati kati ya Jiji la Dar es Salaam.







All the contents on this site are copyrighted ©.