2013-03-30 15:34:50

Rais Kenyatta na William Ruto washinda kesi ya uchaguzi mkuu!


Mahakama kuu ya Kenya katika kikao chake kilichofanyika Jumamosi, tarehe 30 Machi 2013 chini ya Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, imetamka wazi kwamba, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mgombea mwenza William Ruto wamechaguliwa kihalali. Uamuzi wa Mahakama kuu ya Kenya umekata mzizi wa fitina kutokana na madai yaliyokuwa yametolewa na Mgombea Urais Raila Odinga.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanabainisha kwamba, kesi hii ilikuwa ni kipimo nyeti cha demokrasia, utawala sheria, amani na utulivu nchini Kenya. Ni matumaini ya wapenda amani kwamba, wananchi wa Kenya sasa watashikamana ili kujenga na kuimarisha umoja wa kitaifa na kukataa katu katu kugawanywa kwa misingi ya ukabila, kama ilivyokuwa inajitokeza wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.







All the contents on this site are copyrighted ©.