2013-03-30 08:58:21

Jengeni utamaduni wa kuheshimiana na kuvumiliana, ili kudumisha haki na amani!


Askofu Mkuu Amoni Kinyunyu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, amesema anaishangaa Serikali kwa kuendelea kukaa kimya kutokana na kuvunjika kwa amani kiasi cha kutishia maisha na vitendo viovu wanavyofanyiwa Viongozi wa Dini na Makanisa yao.

Askofu Kinyunyu alisema hayo katika Ibada ya Alhamisi Kuu, 28 Machi 2013, alipokuwa akitoa Baraka kufuatia Semina ya Mahubiri ya Pasaka yaliyofanyika Usharika wa KKKT, Dodoma, ambapo Wakristo walikuwa wakifundishwa Maana ya Alama ya Msalaba kama ilivyo katika Barua ya kwanza kwa Wakorintho 1:18.

“Kwa sababu Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni Nguvu ya Mungu”.alisema Mtume Paulo akiwaambia watu wa Korintho ambao leo ni Mimi na Wewe.

Askofu Kinyunyu alisema, vitendo vya Kinyama ambavyo wamekuwa wakifanyiwa Viongozi wa Dini hasa zaidi wa Kikristo na Waislam wanaoiisema kweli na kukemea Maovu bila kubabaisha, imeonekana kuwa tishio la uhalifu na mafanikio batili ya waovu hao hivyo kuamua kufanya mauaji kama kurudisha Kisasi.

Aliongeza kwamba, Ingawa kusudi na nia ya wahalifu hao ni kutaka Kanisa na Waamini waadirifu Waone na kuamini kuwa Serikali na Waislam ni maadui ili Kanisa kwa namna nyingine nalo lilipize kisasi cha kuchomewa Makanisa na kuuwawa na kujeruhiwa kwa Viongozi wake, limeshindwa.

Kinyunyu aliwaasa wakristo kuwa, kama vile Yesu Kristo alivyosema kwa waliomsulubisha Msalabani, Hata Kanisa liwasamehe wanaolifanyia uovu Taifa Nyamavu la Wakristo nchini Tanzania kwa sababu Biblia inasema Kisasi ni kwa ajili Mungu mwenyewe.

Hata hivyo alionya kwa watendao maovu hayo na Serikali inayosimamia amani inayokaa kimya kwamba waelewe kisasi cha Mungu ni kibaya kuzidi ngurumo na radi, kuzidi mamlaka ya kibinadamu, amlaka ya Kirumi na Kiyahudi, kwa kuwa ahadi ya Mungu katika Biblia Warumi.8:37-38; inasema, “Kama ilivyoandikwa ya Kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tunahesabiwa kuwa kama Kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika Mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda.

“Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala Malaika, wala Mamlaka, wala yaliyopo, yatakayokuwapo, wala yaliyopo juu, wala yaliyopo chini, wala kiumbe kinginecho, chote, hakitatutenga na upendo wa Mungu wetu ulio katika Kristo Yesu Bwana Wetu”.

Aidha alimaliza kwa kusema, Wakristo wasiwachukie Wa-Islam kwa sababu kama wapo wanaolfanyia Kanisa matendo hayo Maovu, si Waislamu waote bali ni kikundi cha baadhi yao ambacho pengine hakina hata Ibada ya kumwogopa Mungu, ila kinaendeshwa na Shetani ambaye ni muongo na mharibifu.








All the contents on this site are copyrighted ©.