Rufaa ya Makanisa ya Oceania kwa haki za Kijamii na uadilifu wa uumbaji
Baraza la Makanisa la Kiekumene la Oceania Pacific, (PCC) katika mkutano wake wa kumi,
ulio malizika hivi karibuni mjini Honiara, limetoa wito na rufaa kwa watu wote, kujali
na kuheshimu haki za binadamu na ulinzi wa mazingira. Tamko kutoka Baraza hili
lenye kujumuisha jumuiya za kidini 34 , lililonukuliwa na gazeti la L'Osservatore
Romano, ambamo wajumbe wa Baraza wametoa wito kwa mamlaka za kimataifa, kutumia njia
zote muhimu, kukuza maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwa watu asilia,
ikiwemo ulinzi na usalama wa mazingira unaowekwa hatarini na mabadiliko ya hali
ya hewa yanayo endelea. Miongoni mwa masuala kushughulikiwa yenye kuleta madhara
katika mazingira na watu, ni majaribio ya kijeshi yanayotumia silaha ya nyuklia,
yanayo fanywa katika baadhi ya maeneo ya Pacific. Jumuiya za kidini zimetoa wito
wa kudai fidia kwa uharibifu unao fanyika. Wajumbe katika mkutano pia alielezea tatizo
la uchafuzi unaofanywa na mitambo ya machimboya madini, na kuzitaka serikali katika
mkoa huo wa Pacific, kuwa na mshikamano na watu ambao wanakabiliwa na athari hazi,
zinazotokana na shughuli za madini,hasa katika mazingira ya baharini. Pia wametaja
matatizo yanayo sababishwa na wavuvi wa kimataifa kutoka nje,ambao wameonyesha kutojali
uharibifu wanaoufanya isipokuwa kutafuta faida zao binafsi. Watu wa Pacific wanakemea
uharibifu huo waksiema, ni kuyaharibumaisha ya watu katiakmkoa huo kwa kuwa mazingira
ya bahari ni chanzo kikuu cha chakula na ustawi wake kiuchumi. Mwisho wamependekeza
ukuzaji wa heshima kwa utu wa watu walioambukizwa virusi vya ukimwi, na pia utoaji
wa msaada kwa watu walio yahama makazi yao, wakikimbia hatari za vurugu za utumiaji
wa silaha zinazo shamirishwa na kuenea kwa silaha, toka nje.
Wajumbe wa Baraza
hili pia waliutumia muda wa mkutano huo, kutoa michango na tafakari na kupendekeza
mada za kupelekwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) utakaofanyika
wakati wa kipindi cha vuli kwa mwama huu, huko Busan, Korea. Na ujumbe wa Katibu
Mkuu wa WCC,Mchungaji Olav Fykse, kwa ajili yamkutano hua, umeonyesha shukrani kwa
ajili ya masuala yaliyozungumzwa wakati wa mjadala. Na kwamba, wako katika maandalizi
ya Mkutano huo wa mwaka wa Busan. Na mawazo mengi yaliyo pendekezwa na CCP, yatajadiliwa
kwa usahihi zaidi katika Mkutano wa Busan, ambamo kituo cha mkutano, ztakuwa mandhari
ya haki, amani na uadilifu katika uumbaji, chini ya kaulimbiu ya amani.