Urafiki na kuheshimiana ni vigezo muhimu kwa watu watamaduni mbalimbali za kidini
Hotuba ya Papa kwa wawakilishi wa Makanisa na Jumuiya za kikanisa na dini zingine.
Jumatano Baba Mtakatifu Francis, alikutana na wawakilishi wa makanisa , jumuiya
za Kikristu na dini zingine, ambao walikuwa wamefika Vatican kwa nia ya kushiriki
katika Ibada ya Misa, aliyoiongoza, kwa nia ya kuzindua utume wake kama kiongozi Mkuu
wa Kanisa Katoliki wa 266 tangu kwa Petro Mtume. Papa Francis, kwa wawakilishi
hawa, ilisisitiza umuhimu wa kukuza urafiki na heshima kati ya wanaume na wanawake
wa mila za dini mbalimbali. Na alitaka dunia daima kudumisha hamu ya kuwa na imani
kwa Ukuu wa Mungu, muumbaji wa vyote vilivyo hai, na kuzikataa tamaa za kutaka kujitukuza
na kumdharirisha binadamu kama vile ni kiumbe au bidhaa iliyo tengenezwa na binadamu.
Kabla ya Mkutano huu, Papa kwanza alikukutana na wawakilishi kadhaa binafsi
akiwemo Patriaki wa Kiekumene wa Constatinople, Bartholomayo I, na Askofu Mkuu Hilarion,
mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Nje Kanisa wa Upatriaki wa Moscow.
Papa
Francis aliianza hotuba yake kwa kuwashukuru wote waliokuwepo kwa nia yao ya kutaka
kumsindikiza wakati akianza utume wake kama Askofu wa Roma, na mrithi wa Petro. Alikiri
kuusikia uwepo wa kiroho wa jumuiya wanazo wakilisha na hivyo kupatwa na hisia
za kutaka kushiriki hata haraka zaidi katika maombi kwa ajili ya umoja wa waumini
wote wa Kristo. Papa alisema, mabadiliko binafsi katika uhusiano na Yesu Kristo,
Mwana wa Mungu, aliyekufa na kufufuka kwa ajili ya wokovu wetu," ni muhimu kwa kila
Mkristo. Na hamu hii ya kutaka kuutangaza ujumbe huu ni kiini cha Mtaguso Mkuu wa
Pili wa Vatican, , ambao una maana sana hasa katika safari ya kiekumeni.
"Tunaomba
Baba mwenye huruma na kutuwezesha kuishi kikamilifu imani kwamba tumepokea kama zawadi
katika siku ya Ubatizo wetu, uwezo wa kutoa ushuhuda wetu kwa uhuru, furaha na ushupavu.
" Na kwamba kwa kadri tunavyo zidi kuwa aminifu kwa mapenzi yake - katika mawazo,
katika maneno na matendo ndivyo tunavyojitahidi kuwa wakweli katika kutembea pamoja
kuelekea umoja kamili", Papa Francis aliomba na kusisitiza.
Na akiwageukia
wawakilishi kutoka dhehebu la Wayahudi, Papa alizungumzia hasa kiungo maalum cha Kiroho,
kati ya Wakristu na Wayahudi. Na alionyesha imani yake kwamba, majadiliano kati ya
Kanisa na Wahayudi, yaliyokwisha anzishwa yataendeela na kutoa matunda mema kama ilivyo
tazamiwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, majadiliano ambayo mpaka yameonyesha
mafanikio mengi na matunda mengi, hasa katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita."
Papa
Francis , kisha alitaja umuhimu wa mazungumzo kati ya madhehebu, akisema, "Kanisa
Katoliki linafahamu na kutambua umuhimu wa kukuza urafiki na heshima kati ya wanaume
na wanawake wa mila tofauti za kidini. Kwa ufahamu huo, Kanisa linaona ni wajibu
ambao kila mmoja wetu anapaswa kuuzingatia kama dira ya kumwongoza binadamu katika
kuvipenda viumbe vyote vya Mungu na kuvilinda. Aliasa, “tunaweza kufanya mengi
kwa ajili ya wale ambao wako katika mazingira magumu , ambao kwa bahati mbaya ni
dhaifu au wale wanaoteseka kupitia ukuzaji wa haki na kuimarisha maridhiano na
kujenga amani." "Lakini juu ya yote," Papa Francis alihitimisha hotuba yake, ni lazima
kuweka hai katika ulimwengu wetu, kiu ya kumtafuta Mungu, na kutoruhusu maono ya binadamu
katika mwelekeo wake mmoja kutaka kujitukuza na kutawala, mwelekeo wa mtu kupuuzwa
na kuwa kama kitu cha kutengenezwa na binadamu au kama bidhaa nyingine anazozitumia
binadamu. Hili ni jambo la hatari zaidi katika nyakati zetu, ameasa Papa Francis.