2013-03-21 15:13:30

Papa Francis atuma Salaam za Matashi mema kwa Askofu Mkuu Justin Welby


Baba Mtakatifu Francis, Jumatatu iliyopita, alipeleka Salaam za matashi mema kwa Askofu Mkuu Justin Welby, wa Canterbury, Mkuu wa Jumuiya ya Waanglikani duniani.
Katika salaam hizo, Papa alianza na Maneno: Neema na amani ya Bwana zimiminwe kwako. Na aliendelea kutoa shukurani zake za dhati kwa Askofu Mkuu Justin, kwa maneno yake mazuri aliyomtumia mara bada ya kuchaguliwa. Hivyo nae, anapenda kujibu salaam hizo, kwa kumtakia kila la heri katika utume wake kama Askofu Mkuu wa Kanisa kuu la Canterbury, na Kiongozi Mkuu wa Wanglikani duniani.
Na kwamba utume wa Kichungaji ni wito katika kutembea kwa uaminifu wa Injili ya Bwana Yesu Kristu. Na amemhakikishia sala zake katika wito wake huu mpya, ulio dhaminishwa kwake na Bwana wenyewe.
Papa anatazamia, wataweza kukutana muda si mrefu , kwa nia za kuendelea kutia joto katika mahusiano ya kidugu yaliyofurahiwa na watangulizi wao.









All the contents on this site are copyrighted ©.