2013-03-21 15:11:27

Kazi kubwa inayo msubiri Papa Francis.....


Patriaki Bartholomew I, kiongozi Mkuu wa Kanisa la Kiotodosi Upatriaki wa Constatinople, akitoa salaam zake za matashi mema kwa Papa Francis, amesema, katika jina la Bwana mwenye uweza, aliyevuvia roho wa Mungu, uchaguzi uliokuchagua wewe, kuwa Khalifa wa Mtume Petro na hivyo kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki la Roma, ambalo limekuwepo tangu nyakati za kale likihudumia kwa upendo mkuu, tunakupokea kwa moyo mkujufu na furaha.

Na unaichukua nafasi hii kutoka kwa mtangulizi wako, Mpendwa Papa Benedict XVI, mtu anayejulikana kwa upole, maarifa na ujuzi mwingi katika teolojia na mwenye upendo, na roho ya ujasiri, ambaye hivi karibuni amejiuzuru katika utume huu kwa sababu za kiafya na uchovu, na hivyo tunaimani nawe.

Pariaki aliendelea kumkumbusha Papa mpya, juu ya kazi na majukumu makubwa yanayomsubiri ya kuwaongoza watu mbele ya Mungu na watu. Na kwamba, umoja wa makanisa ya Kikristo ni hatua ya kwanza na muhimu zaidi kuwezesha Wakristu kama wafuasi wa Kristu mmoja , kutoa ushuhuda wa imani dhahiri na kuaminika katika macho ya wale walio karibu na mbali. Kwa ajili ya kufanikisha umoja huo, ni muhimu kuendeleza mazungumzo ya kiteolojia, ambayo tayari yalikwisha anzishwa, ili ukweli wa imani na uzoefu wa Watakatifu, watu wa Mungu na mapokeo ya kawaida kwa Mashariki na Magharibi, wa tangu millenia ya kwanza ya Ukristo kwa pamoja viweze kueleweka na kukaribiana kama usharika mmoja.

Ni mazungumzano yanayo endelezwa kwa upendo na ukweli katika roho ya unyenyekevu na upole, nguvu na silaha ya silaha za kweli, katika majadiliano haya. Na kwamba mgogoro wa uchumi duniani, kwa upande mwingine, unahitaji kuangaliwa kwa haraka na kwa makini, kwa ajili ya ufanikishaji wa huduma za ubinadamu, ambazo Yeye Papa Francis anao uzoefu mkubwa katika ufanikishaji wake , kwa kuwa amekuwa akijihusisha na hilo kwa muda mrefu, kama msamaria mwema huko Amerika ya Kusini, na hivyo anakuwa kati ya wachungaji wema wachache wanaojali uchungu wa mateso na taabu ya binadamu.

“Tuna wajibu wa kulisha wenye njaa, kutoa mavazi kwa walio uchi, na kuponya wagonjwa na kwa ujumla hofu juu ya wale walio katika haja, kwa kuwa anastahili kusikia kutoka kwa Bwana. "Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari."

Na kwamba, Papa Francis kuchagua unyenyekevu, Utakatifu na fadhila , kumeonyesha dhahiri kwamba, vitakuwa ni vigezo muhimu vitakavyo ongoza utawala wake . Hili limejaza moyo wa matumaini katika mioyo ya watu wengi, waliotawanyika kote duniani. Parriaki Batrholomew I, ameendelea kuonyesha imani yake kwamba, Utawala wa Papa Francis, haki na huruma, vitaweza kuwakilisha mahitaji muhimu kisheria, kwa ajili ya Kanisa, katika umuhimu wake kwenye msingi maadili na mastahili.

"Tunaomba kwa moyo wote, pamoja na Wakristo wote amini duniani kote, na kwa ajili ya binadamu wote kwamba, utawala wako uwe na mafanikio makubwa katika utume huu mgumu na muhimu kwa ajili ya binadamu wote".
Mwisho Patriaki Bartholome I, alimwombea Papa Francis Baraka na Neema kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo na Utukufu kwa Mungu, ambaye kila nyakati huchagua watumishi wake wanao stahili kutembea katika njia ya wito wake, unaowaongoza wanadamu katika wa utukufu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina.








All the contents on this site are copyrighted ©.