2013-03-19 15:10:38

Papa Francis, ahimiza kila binadamu anao wajibu wa kulinda na kutunza viumbe na yote yaliyo mema na mazuri.


Baba Mtakatifu Francis , akihutubia wakati wa Ibada maalum ya kuzindua kazi zake za Kitume kama khalifa wa Mtume Petro , amemshukuru Mungu kwa majaliwa yake, yaliyomwenzesha kuifikia siku hii maalum kwake, ikienda sambamba na Siku Kuu ya Mtakatifu Yosef, Mchumba wa Bikira Maria na mlinzi wa Kanisa la Ulimwengu.

Alisema, Wapendwa ndugu zangu wake kwa waume, ninamshukuru Bwana kwa kuniwezesha kusherehekea Ibada hii ya Misa Takatifu, kwa ajili ya uzinduzi wa utume wangu , sambamba na sikukuu ya Mtakatifu Joseph, Mchumba wa Bikira Maria na mlinzi wa Kanisa zima. Na pia imekuwa ni muhimu kwamba, ni siku ya wajina wa mtangulizi wangu, Josef Ratzinger , ambaye tupo karibu nae kupitia sala zetu za upendo na shukrani.

Papa aliendelea kutoa salaam zake za upendo wa dhati kwa ndugu zake Makardinali , Maaskofu, Mapadre, Mashemasi, Watawa wa kike na kiume na kwa wote walio yatolea maisha yao wakfu. Na pia aliwashukuru wawakilishi wa Makanisa mengine na Jumuiya za kikanisa, pamoja na wawakilishi wa jamii ya Wayahudi na jumuiya nyingine za kidini, kwa uwepo wao. Salamu pia alizitoa kwa Wakuu wa Nchi na Serikali, vyama na na Wajumbe rasmi kutoka nchi nyingi ulimwenguni kote, na Mabalozi.

Papa akitafakari somo la Injili alieleza jinsi Mtakatifu Yosefu, alivyo fanya kama alivyomwambia na malaika, mchukue Maria kama mkeo, (Mt 1:24). Papa amesema, Maneno haya tayari yanaonyesha utume ambayo Mungu aliudhaminisha kwa Yosefu: kuwa mlishi na mlinzi Kanisa la Kristu. .

Papa aliendelea kutafakari dhamana hii ya Yosef kwa Maria na Yesu, akisema, katika ukweli wake, inapanuka na kuwa mlinzi wa Kanisa zima, kama Mwenye Heri Yohane Paulo II alivyosema: "Kama jinsi Mtakatifu Yosefu alivyo mhudumia kwa upendo wa Maria na kufurahia dhamana ya kumlea Mtoto Yesu, anawekwa wakfu wa kulilinda fumbo la mwili wa Kristu ambalo ni Kanisa, ambamo Bikira Maria ni mfano wa kuigwa "(Redemptoris Custos, 1).

Papa Francis, aliendelea kueleza kwa jinsi gani Yosef anaitikia wito huu wa kumlinda Maria , Yesu na Kanisa, akisema, daima anakuwa ni mfano wa kuigwa katika uangalifu wa kusikiliza sauti ya Mungu, katika kujifunua wazi kwenye ishara za uwepo wa Mungu, na utayari wa kuipokea mipango yake , na si kwa kufuata nia zetu tu.

Pia alitoa maelezo kwa jinsi Yosefu alivyopokea jukumu lake kama mlinzi kwa siri, kwa unyenyekevu na ukimya, tena kwa uaminifu mkubwa, aksiema hata pengine, inakuwa vigumu kuelewa. Aliaja matukio makubwa yaliyotajwa katika mtiririko wa historia ya wokovu wa binadamu kama yanenavyo maandiko Matakatifu juu ya Yosef, tangu wakati wa uchumba, kuoana , kwenda kuandikishwa Bethlehemu wakati wa Sensa, kuzaliwa kwa Yesu, kukimbilia Misri, kutafutwa kwa Yesu Hekalini wakati akiwa na miaka kumi na mbili, na baadaye katika maisha siku hadi siku wa nyumbani mwao Nazareti, ambamo alimpa Yesu majiundo katika kazi zake za uselemara na malezi mengine kwa mujibu wa mila na desturi za kiyahudi.

Papa amefafanua kwamba, hii inaonyesha jinsi gani Yusufu aliweza kuitikia wito wa kuwa mlinzi wa Mariamu, Yesu na Kanisa. Daima alikuwa makini katika kuisikiliza sauti ya Mungu, ishara ya uwepo wa Mungu na kupokea mipango ya Mungu, na si tu kwa faida yake mwenyewe, lakini kwa ajili ya manufaa ya wengine. Na kama ilivyokuwa kwa Daudi, kama ilivyosikika katika kusoma kwanza. Mungu hataki nyumba iliyojengwa na watu , ila katika uaminifu neno lake, na kwa mpango wake. Mungu mwenyewe ambaye hujenga nyumba, kutoka katika mawe hai yaliyotiwa muhuri na Roho wake.

Kwa Yosef, Papa anasema, tunajifunza jinsi ya kuitikia wito wa Mungu, kwa urahisi na kwa hiari , huku tukiuona msingi wa wito wa Kikristo, ambaye ni Kristo! Na tudumishe maisha yetu kwa Kristu ili tuweze kuwalinda wengine, ili tuweze kulinda viumbe, na tuweze kujilinda wenyewe!

Papa ameeleza na kutoa wito kwa kila mmoja kuwa mlinzi, si kwa Wakristu tu , ili kila binadamu awe a mwelekeo huu, akimshirikisha mtu mwingine, mazuri yote ya kuwa walinzi wa viumbe na uzuri wote wa maumbile asilia ya dunia, kama Kitabu cha Mwanzo kinavyo tuambia na kama Mtakatifu Francis wa Assisi alituonyesha, kuheshimu mazingira ambamo tunaishi.

Papa alifafanua , hii inapata pia maana zaidi kwamba, ni utetezi wa maisha ya watu na mahitaji yao , kuonyesha upendo, ukarimu na mshikamano na kujali mahitaji, hasa kwa makundi yaliyo dhaifu zaidi, watoto, wazee na wale wagonjwa, ambao mara nyingi husahaulika. Ina maana ya kujali wengine pia ndani ya familia zetu: waume na wake, kutoa ulinzi kwa mtu mwingine, na kisha, kama wazazi, kuwahudumia watoto, na watoto nao kuwalinda wazazi wao. Ni kujenga urafiki wa dhati, ambamo kila mmoja anawajibika kumjali mwingine kwanza, kujaliana kwa kuheshimiana pia kiimani na katika kutendeana wema, kama zawadi kuu itokayo kwa Mungu!

Papa ameasa kwamba, kila binadamu anayeshindwa kuuishi wajibu huu, huifungua njia za uharibifu na nyoyo ngumu zilizojaa ukatili. Kuukataa wajibu huu wa kujaliana na kurudi katika kipindi nyakati za historia ya kusikitisha, kama ilivyokuwa wakati wa kipindi Herode, ambao njama vifo, uharibifu na maovu yasiyokuwa na kipimo yaliyofanywa mbele ya uso wa wanaume na wanawake.

Kwa maneno hayo, Papa pia aliwageukia wenye mamlaka mbalimbali katika maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, na watu wote, wake kwa wanawake, akiwasihi katika utendaji wao wa kila siku jambo la kwanza wajali kuwa "walinzi" wa uumbaji, walinzi wa mpango wa Mungu kama ilivyo andikwa katika asili, walinzi wa mmoja kwa mwingine na wa mazingira. Na wajiepushe kuruhusu chumvi ya uharibifu na kifo, kuharibu uso wa dunia yetu. Kuwa walinzi, basi, pia ina maana ya kushika kilicho chema katika hisia zetu na ndani ya mioyo yetu, kwa sababu ni sisi hao hao tunaoweza kujenga au kubomoa. Lazima tusiwe na hofu ya kutenda wema, na huruma!

Amesisitiza katika Ibada hii ya kuzindua Utume wake wa Kipapa, ameomba nyota ya matumaini, kuwaangazia wote , ili waweze kuona umuhimu wa kulinda na kudumisha majaliwaya Mungu kwa watu wote. Na kwa maombezi ya Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu, na Watakatifu Petro na Paulo, na Mtaktifu Francis, ili Roho Roho Mtakatifu aweze kuuongoza Utume wake. Na pia ameomba waamini wasimsahau katika sala zao.







All the contents on this site are copyrighted ©.