Baba Mtakatifu Francis azindua utume wake kwa Ibada ya Misa
Jumanne hii majira ya asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na uongozi
wake kwa Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , hapa
Vatican. Papa ameongoza Ibada hii akisaidiana na Makardinali na Maaskofu wapatao 180
na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31 , Viongozi wa Kifalme 6 , Wana Wafalme 3 , Mawaziri
Wakuu 11. Na kumekuwa na umati wa watu wasiopungua 200, 000, watu wa dini na tamaduni
zote. .
Kabla ya Ibada, Papa akiwa ndani ya gari la Kipapa jeupe la wazi,
aliwasiri katika uwanja huu, ambako alipita katika vijia vilivyoandaliwa kuzungukia
kwa ajili ya kusalimia watu wa kariba na dini zote, waliokuwa wakimsubiri kwa hamu,
kabla ya kuanza Ibada. Mara baada ya zoezi hilo, aliingia ndani ya Sakrastia kwa
ajili ya maandalizi ya kuanza Ibada, ya Maadhimisho ya Siku Kuu ya Yosefu Mchumba
wa Maria na mlinzi wa Kanisa la Ulimwengu, na pia kwa nia ya kuzindua utume wa kazi
zake kama khalifa wa mtume Petro.
Papa Francis, akiwa mrithi wa Mtakatifu
Petro wa 265, aliiianza Ibada hii kwa kuteremka chini katika Kaburi la Mtakatifu
Petro , kama yalivyo mapokeo ya tangu kale, akiwa ameandamana na Mapatriaki wa Makanisa
ya Mashariki ambako kwa muda walitolea sala na kufukiza ubani wa kitume.
Baada
ya ya hapo , Papa alijiunga katika maandamano ya kuanza Ibada katika uwanjani wa
kanisa Kuu. , huku sala na maombi mbalimbali yakitolewa......."kwa Papa Francis
Kuhani Mkuu na Askofu wa Roma, ambaye leo hii anauanza utume wake, mjalie nguvu na
uelewa wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya umoja wa Kanisa la Ulimwengu"......
Katika
Ibada hii ya kipekee, Papa Francis, kama Mkuu wa Kanisa la Kristu, khalifa wa mtume
Petro na Askofu wa Roma, alivalishwa Paullium na Pete ya Petro, ishara ya kuuanza
Utume wake..."Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu na milango
ya kuzimu kamwe haitakuzuia . Nitakupa Ufunguo za Ufalme wa Mbingu"........
Palium aliyovaaa Papa , imetengenezwa kwa mayoya ya kondoo , kama ishara ya Askofu
na Mchungaji mwema wa kondoo. Pallium hiyo, juu yake kuna misalaba sita midogo mwekundu,
ikiashiria alama ya mwana kondoo aliyesulubiwa kwa ajili ya wokovu wa binadamu.
Na hivyo inakuwa tofauti kidogo na Pallium wanayovalishwa Maaskofu Wakuu ambayo huvaa
pallium yenye misalaba midogo sita mweusi inayoashiria mwana kondoo mpotevu na dhaifu
anayebebwa mabegani na kupelekwa katika maji ya uzima .
Wakati Papa akiwavlishwa
Pallium manaeno haya yalisema, Mungu wa amani , aliyemfufua kutoka katika wafu Bwana
wetu Yesu Kristu, Mchungaji Mkuu wa wanakondoo na akuvalishe Pallium hii iliyo inayotoka
katika Kaburi la Mtakatifu Petro.
Mchungaji mwema aliyempa Petro mamlaka
ya kulisha wana kondoo wake. Leo hii wewe unakuwa mrithi wa Petro, kama Askofu wa
Kanisa hili ambamo Mtume Petro na Paulo walikuwa ni Mababa wa Imani.
Roho
wa Ukweli , anayetoka kwa Baba na akijualie wingi wa zawadi ya hekima na maarifa katika
kuzitenda kazi zake za kitume na hasa katika kuwaimarisha waamini kiroho na katika
umoja wa Kanisa. .......
Baada ya kuvalishwa Pallium, Papa alivalishwa Pete
ya Petro. Pete inayoitwa Pete ya mvuvi , kwa sababu Petro Mtume alikuwa ni Mvuvi.
Petro baada ya kumwamini Kristu, alifanywa kuwa mvuvi wa watu na Kristu mwenyewe.
Na hivyo unakuwa ni wito kwa Mkhalifa wote wa Mtume Petro, kuwa mstari wa mbele kuteka
nyavu za Injili ya wokovu kilindini, kuvua wake kwa waume kwa Injili ya Kristu.
Papa
alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikifuatiwa na sala " , Kristu
Mwana wa Mungu aliyehai , Mchungaji na Mlinzi wa roho zetu, aliyelijenga kanisa lake
juu ya mwamba huu, anakupatia pete ya Petro iliyotiwa muhuri wa Peter Mvuvi wa Galilea,
ambaye Bwana alimpa dhamana ya kutunza funguo za Ufalme wa Mbinguni.
Leo hii,
unakuwa Khalifa wa Mtume Petro , Askofu wa kwanza wa Kanisa lilojengwa katika umoja
wa Upendo , kama Mtume Paulo pia alivyofundisha. Roho wa Upendo na amiminwe ndani
ya mioyo yetu , na akujalie upole na uimara wa kudumisha kupitia utume wako, wale
wote wanaosadiki katika ushariki wa Kristu". ......
Pia Makardinali wawili
kwa niaba ya dekania ya Makardinali wote walionyesha heshima na utii wao kwa Papa
mpya Francis kwa maneno , , Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu, nitalijenga Kanisa
langu , na milango ua kuzimu haitakuzia. Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbingu . Kila
utakalo liruhusu duniani na mbinguni litabarikiwa na kila utakalo lifunga duniani
na mbinuni litafungwa .
Kilichofuatia ni Liturujia ya Neno, masomo yaliyoandaliwa
kwa ajili ya Siku Kuu Mtakatifu Yosef, Mchumba wa Bikira Maria. Somo la kwanza kutoka
Kitabu cha Samweli 7, 4-5, 12-14. 16 , Somo la pili kutoka Barua ya Mtume Paulo kwa
Warumi 4: 13,16-18.22 na Somo la Injili ya Marko 1:16, 18-21, 24 a.