2013-03-16 07:45:56

Serikali ya Tanzania yatuma salam za pongezi kwa Papa Francis


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Ijumaa 15 Machi, 2013 amemtumia salamu za Pongezi Baba Mtakatifu Francis kwa kuchaguliwa kwake kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki.

“Kuchaguliwa kwako ni ushuhuda tosha wa imani na heshima kubwa ambayo Kanisa Katoliki inayo kwako, historia yako na upendo wako wa kujali na kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa Wakatoliki, wasio Wakatoliki na wasio Wakristo pia kusherehekea uteuzi wako” Rais Kikwete amesema kwenye barua yake ya Pongezi kwa Papa Francis .

Vatican na Tanzania imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete amemhakikishia Papa Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia utaimarika zaidi chini ya uongozi mpya wa Papa Francis.








All the contents on this site are copyrighted ©.