2013-03-15 09:08:04

Papa kuanza utume wake rasmi kama Khalifa wa Mtakatifu Petro hapo tarehe 19 Machi 2013


Baba Mtakatifu Francis amemwandikia barua Rabi mkuu wa Roma Riccardo di Segni, akimjulisha rasmi kwamba, tarehe 19 Machi 2013 ataanza rasmi utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francis kwamba, atachangia katika kuendeleza mchakato wa uhusiano mwema kati ya Wayahudi na Wakatoliki, uliotolewa na Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican; kwa ajili ya kushirikiana katika huduma ili kuleta mabadiliko duniani, daima wakijitahidi kutekeleza mapenzi ya Mungu.







All the contents on this site are copyrighted ©.