2013-03-15 11:00:06

Maaskofu DRC watuma salam na matashi mema kwa Papa Francis


Familia ya Mungu nchini DRC imepokea kwa furaha na moyo mkuu taarifa za kuchaguliwa kwa Kardinali Jorge Mario Bergolglio kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Katika ujumbe uliotiwa sahihi na Askofu Nicolas Djomo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki DRC unasema kwamba, kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu Francis ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Kanisa na Dunia kwa ujumla wake.

Baraza la Maaskofu Katoliki DRC kwa niaba ya Familia ya Mungu nchini humo, linamtakia kheri na baraka Baba Mtakatifu Francis katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa amsindikize katika hija ya utume wake kwa Kanisa la Kiulimwengu.







All the contents on this site are copyrighted ©.