2013-03-14 07:51:49

Salam na matashi mema kwa Baba Mtakatifu Francis wa kwanza kutoka Argentina!


Dr. Cristina Fernandes de Kirchner, Rais wa Argentina, kwa niaba yake mwenyewe na kwa niaba ya Serikali ya Argentina, amemtumia salam za matashi mema na pongezi Baba Mtakatifu Francis kwa kuteuliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki.

Ni matumaini ya wananchi wa Argentina kwamba, Baba Mtakatifu ataweza kutekeleza wajibu na dhamana yake kama Kiongozi wa Kanisa, utume ambao utamwezesha kuzaa matunda katika mchakato wa kutafuta haki, amani, usawa na udugu kwa ajili ya binadamu wote.







All the contents on this site are copyrighted ©.