2013-03-14 14:49:13

Pongezi za COMECE kwa Papa Mpya


Tume ya Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki la Ulaya( COMECE), kwa furaha imeungana na familia ya Kanisa la Ulimwengu, kumpongeza Papa Mpya , Muadhama Jorge Maria Kardinali Bergolio, kwa kuchaguliwa na kuchukua jina jipya la Papa Francis.
Padre Patrick H. Daly, Katibu Mkuu wa COMECE, akitoa pongezi hizo, anasema, tangu mwanzo , Tume imekuwa ikifurahia msaada wa kazi na maslahi ya watangulizi Papa Mpya, ambao wote walifuatilia kwa ukaribu, maendeleo ya kanisa katika Umoja wa Ulaya.

Na kwa wakati huu, ambamo kuna utata wa kina kuhusu mustakabali wa Ulaya, inakuwa ni wakati muafaka kwa Papa mpya kuingiza shauku mpya za utendaji unao tafuta mwelekeo mpya wa Ulaya, wenye kukumbatia tunu za Kikristo, zilizo vuviwa na waanzilishi wa Umoja wa Ulaya.
Padre Daly ameeleza na kurejea barua ya Kitume maalum kwa ajili ya Ulaya, iliyotolewa na Mwenye Heri wa Yohane Paulo II, iliyochapishwa miaka kumi iliyopita, ambayo ujumbe wake bado una nguvu kwa wale wanaofanya kazi ya kuunda sura mpya ya Ulaya ya kesho.mbua na kuendeleza kile kilicho kwisha fanikishwa, katika utendaji wa pamoja na Mataifa ya Ulaya. Na pia atawahimiza Viongozi wa Kisiasa Ulaya na watendaji wote katika COMECE – kudumisha mshikamano na ushirikiano, hasa katika wakati huu wa kutembea pamoja katika njia inayofafuta umoja kamili, licha ya tofauti nyingi za utamaduni na mila ndani ya familia ya watu wa ulaya.

COMECE , ni tume ya Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Ulaya inayoundwa na Maaskofu 26, wakiwakilisha mataifa yote wanachama wa Umoja wa Ulaya . Na kwa zaidi ya miaka 30 , COMECE, imekuwa ikihusishwa katika taratibu za kujenga na kuimarisha mshikamano wa mataifa ya Ulaya . COMECE pia kwa wakati huu ni mbia wa Taasisi za Umoja wa Ulaya zinazoshughulika na majadiliano juu ya utendaji wote wa mataifa ya Ulaya.

Pongezi za ACLI
Gianni Bottalico , Rais wa chama cha Wakristu wafayakazi Italia (ACLI) mara baada ya Kardinali Jorge Mario Bergolia kutangazwa kuwa Papa Mpya, akiungana na waumini wote na watu wenye mapenzi mema kwa ajili ya uchaguzi wa Papa Mpya , alionyesha furaha na matumaini juu ya kuchaguliwa kwa Kardinali Jorge Mario Bergolio, Papa mpya ambaye kwa sasa jina la Kipapa, naitwa Papa Francis.
Sura ya Papa Mpya anaendelea kusema Bottalico ,inajionyesha si tu kama mtawala wa kipekee, bali ina sura ya baba mwema , mchungaji na mwalimu, aliyeyatolewa maisha yake yote katika kumfuata Yesu, katika njia kuu ya mtaguso mkuu wa Vatican, mwongozo na uthibitisho wa imani, kwa ndugu zake wanaotembea katika barabara ngumu leo hii duniani.

Baada ya ishara za uhuru na upendo, zilizoonyeshwa na Mstaafu Benedict XVI katiak nyaraka zake mbalimbali, kuchaguliwa kwa Papa Francis, anasema Bottalico, kunaonyesha mwendelezo wa imani kwamba Askofu wa Roma, Khalifa wa Petro, anaitwa kueneza na kusimamia Injili ya Kristu kwa wakati wote na kwa upendo mkuu. Kwa mtazamo huo, ameweka matumaini yake ya Askofu mkuu wa zamani wa Buenos Aires, Mjesuit wa kwanza, kuingia katika historia Mapapa,na hisia kwamba ataendelea kuwa mtetezi mkuu wa haki ya kijamii na kwa ajili ya ukombozi wa maskini: hasa katiak maeneo yanayoraruliwa na migogoro ya kijamii si tu katiak taifa lake la Argentina, lakini kama hoja inayohitaji utatuzi wa kimataifa.

ACLI, inamhakikishi Papa Mpya, kuwa itatenda kwa uaminifu, moyo wa unyenyekevu na upendo, katika mafundisho yake yatakayo kuw ayakichupuliwa na imani katika Injili ya Kristu, hasa ktiak ufanikishaji wa demokrasia kwa wafanyakazi , kwenye mwendelezo wa uzoefu wa utendaji wa kila siku na majitoleo ya kimwili na kichumi,kwa mujibu wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa, yenye kujali matatizo misingi ya binadamu.
Nayo Uingereza na Wales.
Askofu Vincent Nichols , Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Uingereza na Wales, ametaja furaha ya Kanisa katika eneo, kufuatia kuchaguliwa kwa Papa Francis, anayekuwa Khalifa wa Mtume Petro wa 266. Amemhakikishia Papa Mpya, majitolea ya sala,msaada na ukarimu wa jumuiya ya Waktoliki wote wa Uingereza na Wales.








All the contents on this site are copyrighted ©.