Matarajio ya Kiekumene baada ya uchaguzi wa Papa Francis
Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli amemtumia
salam na matashi mema Baba Mtakatifu Francis, kwa kusema kwamba, huduma yake ya kitume
kama Khalifa wa Mtakatifu Petro, itasaidia kudumisha mchakato wa kutafuta amani duniani
pamoja na kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini, magonjwa na ujinga.
Ni matumaini
yake kwamba, Baba Mtakatifu Francis ataendeleza mchakato wa majadiliano ya kiekumene
miongoni mwa Makanisa haya mawili.