2013-03-14 11:19:48

Kuomba sala na baraka kutoka kwa waamini ni tendo cha unyenyekevu wa Kiinjili!


Di Holger Milkau, Dekano wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri nchini Italia, ametuma salam za pongezi na matashi mema kwa Baba Mtakatifu Francis kwa kuteuliwa kwake kuliongoza Kanisa, kielelezo cha mchakato wa mageuzi yaliyoanzishwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita.

Kitendo cha Papa kupiga magoti na kuomba sala na baraka kutoka kwa waamini kunaonesha moyo na ari ya Kiinjili. Ni dalili za ushuhuda wa imani unaowagusa waamini wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri. Ni matumaini yake kwamba, Baba Mtakatifu Francis ataendeleza moyo na ari ya majadiliano ya kiekumene, katika ukweli na uwazi pamoja na kuendeleza mshikamano wa Kiinjili miongoni mwa Makanisa haya mawili.







All the contents on this site are copyrighted ©.