Hali ya wananchi wengi wa Kenya baada ya uchaguzi inategemea uwajibikaji makini wa
wanasiasa!
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon amewapongeza wananchi wa Kenya kwa
kushiriki kwa wingi na hatimaye, kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi mkuu uliofanyika
hapo tarehe 4 Machi 2013 kwa amani na utulivu na kuyapokea pia matokeo kwa hali ya
utulivu, hizi ni dalili za ukomavu wa kidemokrasia na utawala wa sheria.
Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza kwa njia ya Simu na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
pamoja na Bwana Raila Odinga, aliyewahimiza viongozi hawa wawili kuhakikisha kwamba,
wanawatuliza mashabiki wao na kwamba, ikiwa kama kuna mtu akuridhika na matokeo ya
uchaguzi badi, akate rufaa kwenye Mahakama kuu, ili haki iweze kupatikana kwa njia
ya sheria.
Hali ya wananchi wengi wa Kenya inategemea kwa namna ya pekee uwajibikaji
wa viongozi wa kisiasa nchini humo. Kwa mara ya kwanza asilimia 86% ya wananchi wa
Kenya waliojiandikisha kupiga kura walishiriki katika zoezi hili la kidemokrasia.