2013-03-12 11:42:11

Mgawanyiko wa Boko Haram unatishia usalama na maisha ya watu Kaskazini mwa Afrika


Askofu mkuu Ignatius Ayau Kaigama, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria anasema kwamba, Kikundi cha Boko Haram kilichokuwa tishio kwa mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, kwa sasa kimesambaratika na kugawanyika katika vikundi vidogo vidogo na kwamba, Kikundi cha "Ansaru" ni kimojawapo! Hiki ni kikundi ambacho kinajihusisha na matukio ya utekeaji nyara na hata wakati mwingine mauaji ya raia wa kigeni, pale madai yao yanaposhindwa kutekelezwa.

Askofu mkuu Kaigama anasema kwamba, mgawanyiko wa Kikundi cha Boko Haram unaendelea kuhatarisha haki, amani na utulivu nchini Nigeria, kwani vikundi hivi kila kimoja kina kiongozi na mikakati yake. Baadhi ya watu walioko kwenye vikundi hivi wamekamatwa nchini Mali, Cameroon na kwamba, kuna hata baadhi ya wananchi kutoka Ufaransa ambao pia ni wanachama wa Boko Haram.

Ili kupata ufumbuzi wa kudumu Serikali ya Nigeria na Umoja wa Afrika hauna budi kushirikiana kwa pamoja ili kujenga na kudimisha misingi ya haki, amani na utulivu!







All the contents on this site are copyrighted ©.