2013-03-09 08:42:16

Conclave inaanza rasmi tarehe 12 Machi 2013


Makardinali katika kikao chao cha nane, kilichofanyika Ijumaa jioni tarehe 8 Machi 2013 wameamua kwamba, mkutano wa kumchagua Papa Mpya utafanyika tarehe 12 Machi 2013. Siku hiyo asubuhi, Makardinali pamoja na Familia ya Mungu kwa ujumla wataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuombea uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican.

Baadaye Jioni, Makardinali wataingia kwenye Conclave, tayari kuanza mchakato wa kumchagua Khalifa wa Mtakatifu Petro.







All the contents on this site are copyrighted ©.