Bado hakuna tarehe ya kikao cha Conclave- Pd Lombardi aeleza
Kikao cha Tano cha Makardinali -bado hakuna tarehe ya kuanza kwa Conclave. Alhamis,
Asubuhi, Makadinali waliendelea na mkutano wao , wakiwa na kikao cha tano, cha kuelekea
Mkutano wa Conclave. Na jioni waliketi katika kikao cha sita. Mkurugenzi wa
ofisini ya Habari Vatican, Padre Federico Lombardi, akitoa muhtasari kwa wanahabari:
juu ya kikao cha tano, alifahamisha kwamba, bado haijulikani tarehe ya kuanza Conclave.
Alitaja idadi ya Makardinali waliohudhuria kikao cha tano kuwa 152. Na kwamba , alikuwa
akikosekana Kardinali mmoja tu mwenye haki ya kupiga kura nae ni Kardinali Pham Minh
Man, wa Vietnam aliyekuwa akitarajiwa kuwasili Alhamis. Padre Lombardi, katika
mkutano huu, aliwataka wanahabari kusikiliza kinachoelezwa na Ofisi ya habari ya Vatican
na kujiepusha na uvumi unaotolewa na wanahabari wasiojua taratibu za mkutano wa Makardinali
Consistori na Conclave, kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyo ripoti juu ya Ibada
za Misa zinazojulikana kwa jina la “Pro eligendo Pontifici ”, wakidhani Ibada hiyo,
itakayoadhimisha Jumatatu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ndiyo mwanzo wa Conclave.
Hiyo si kweli. Padre Lombardi amefafanua kwamba, Ibada hizo za Pro Eligendo Pontifici
zinaweza kuadhimishwa nyingi tu , kwani hutolewa kwa nia za kuombea baraka vikao vya
Conclave. Na hivyo, aliendelea, -“Missa Pro eligendo Pontifice” ni Misa inayoweza
kuadhimishwa na Padre yeyote, katika siku hizi, kwa nia ya kuomba Roho Mtakatifu
alisaidie Kanisa , katika hali hii ya Kiti cha Petro kuwa kitupu. Na hivyo si kila
Ibada ya Missa Pro eligendo Pontifici, huwa na nia ya kufungua vikao vya Conclave. Pia
katika kikao cha Alhamis Asubuhi , walichaguliwa wasaidizi wapya wa watatu wa Camerlengo
, nao ni Kardinali Boutros Rai Patriaki wa Maronite, akiwakilisha Maaskofu Makardinali
, Kardinali Monsengwo kwa Makardinali Mapadre, na Kardinali De Paolis kwa Makardinali
Mashemasi, wote watatu watakuwa wasaidizi wa mstari wa Mbele katika dawati la Camerlengo.
Kazi watakao ifanya kwa muda wa siku tatu . Aidha katika kikao hiki cha Tano,katika
umoja wao kama Decania ya Makardinali walituma salaam zao za rambirambi , Venezuela
, kufuatia kifo cha Rais wa Venezuela Hugo Chavez. Na pia, waliendelea kusikiliza
michango na maoni , kati ya walioshiriki kutoa hoja, kwanza, ni wale wanaohusika na
idara za uchumi , Kardinali Versaldi, Calcagno na Bertello. Versaldi ni Gavana wa
Mambo ya Uchumi, rais wa APSA, Tawala za urithi wa Kiti cha Kitume, na Bertello ni
Rais wa Utawala Vatican. Na kwamba majadiliano yalifanyika katika utaratibu
wa kujali mizania za bajeti, wakianisha ilivyokuwa mwaka uliopita, na matazamio
ya mwaka ujao, na kisha kujadiliwa Makardinali 15 na kuchapishwa katika vyombo vya
habari hapo Julai , ikifuata utaratibu wake uliopo. Pamoja na kujadili mengine
mada ya uinjiishaji wa Kanisa katika ulimwengu wa leo, Kiti Kitakatifu, idara za
Vatican mahusiano na Maaskofu, matarajio na sifa za Kardinali anayefaa kuchaguliwa
kuwa Papa, zinaendelea kupewa kipaumbele na muda zaidi katika vikao .