2013-03-06 07:13:54

Makardinali watuma salam na matashi mema kwa Papa mstaafu Benedikto XVI


Makardinali kwa njia ya simu ya maandishi,, Jumanne tarehe 5 Machi 2013, wamepeleka salam za matashi mema kwa Papa Mstaafu Benedikto XV1 , ambaye kwa wakati huu anaishi Castel Gandolfo , Makazi ya Kipapa yaliyoko nje kidogo ya jiji la Roma. Ujumbe huo unasema:
Kwako,
Papa Mstaafu Benedikto XV1,
Castel Gandolfo.
Makardinali , wakiwa wamekusanyika mjini Vatican kwa ajili ya Mkutano wa kawaida wa maandalizi ya kikao kijacho cha uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro, wanapenda kuchukua nafasi hii kukutimia salaam zao za upendo, kwa mara nyingine wakirudia kutoa shukrani zao za dhati, kwa mwanga wa fumbo la kiti cha Petro na kwa kuwa kwao, mfano wa Mchungaji mwema na mnyenyekevu, kwa ajii ya mafao ya Kanisa na dunia kwa ujumla.
Shukrani zao zinalenga kuonyesha utambuzi wa Kanisa zima kwa kazi ulizofanya bila kuchoka katika Shamba la Bwana.
Umoja wa Dekania ya Makardinali , unaendelea kuweka tumaini katika maombezi yako, kwa ajili yao na kwa ajili ya Kanisa Takatifu.
+Kardinali Andelo Sodano.
Dekano wa Dekania ya Makardinali.
Kutoka Vatican, 5 Mach 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.