2013-03-06 09:51:25

Jumuiya ya Kimataifa inawapongeza Wakenya!


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon, amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kufanikisha mchakato wa uchaguzi mkuu kwa utulivu na uwazi na kwamba, hii inaweza kuwa ni hatua makini kwa Kenya katika ujenzi wa demokrasia, amani na utulivu.

Umoja wa Afrika umeonesha kuridhishwa kwake na hali ya uchaguzi nchini Kenya, uliofanyika katika "hali ya amani na utulivu". Viongozi wanasikitishwa na idadi kubwa ya kura zinazohofiwa kwamba, zimeharibika. Serikali ya Marekani inawataka wananchi wa Kenya kuhakikisha kwamba, malalamiko yote kuhusu uchaguzi yanapatiwa ufumbuzi kwa njia ya sheria, ili kutolitumbukiza tena taifa kwenye maafa kama ilivyojitokeza katika chaguzi kadhaa zilizopita.







All the contents on this site are copyrighted ©.