2013-03-05 11:11:30

Baa la njaa linawanyemelea watu zaidi ya millioni 6 Kusini mwa Afrika


Zaidi ya watu millioni sita, Kusini mwa Afrika wanakabiliwa na baa la njaa. Hawa ni wale wanaopatikana nchini Angola, Lesotho, Malawi na Zimbabwe. Hii ni kutokana na uwepo wa ukame wa muda mrefu na baadaye mafuriko yaliyobabisha maafa na uharibifu mkubwa wa mazao mashambani.

Hayo yamesemwa na Chama cha Msalaba Mwekundu katika kampeni yake ya kutafuta fedha ya msaada kwa waathirika hawa. Licha ya baa la njaa, lakini wananchi wengi pia kwa sasa wanakumbwa na magonjwa ya mlipuko kama vile: Malaria, Kipindu pindu na kuhara.







All the contents on this site are copyrighted ©.